Simba iko tayari kumuuza Kichuya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
23 Oct 2017
Simba iko tayari kumuuza Kichuya
Uongozi wa Klabu ya Simba umemuweka sokoni kiungo mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa kukaribisha ofa kutoka klabu yoyote.

Hivi karibuni Klabu ya Ismailia ya Misri ilishindwana na Simba juu ya dau la kumuuza kiungo huyo ambalo lilikuwa dogo, hivyo kusababisha uongozi wa klabu hiyo kukataa.

Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wanacheza kwa kiwango kizuri na kuisaidia timu yake hiyo, jambo ambalo timu nyingi zimekuwa zikimnyemelea.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amefunguka kuwa, dili lao na Ismailia juu ya kumchukua Kichuya limekufa rasmi, lakini wamemuweka sokoni mchezaji huyo kwa timu yoyote itakayomhitaji.

“Ile dili kati yetu na Ismailia ilishakufa rasmi kwa sasa hakuna ishu ya Kichuya kwenda huko, lakini tupo tayari kupokea ofa yoyote ile, iwapo kuna timu itamhitaji tutakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo.

“Simba tumekuwa na desturi ya kuwaachia wachezaji wetu kuwauza pale tunapofanikiwa kupata timu ya kucheza, hivyo mchezaji yeyote yule atakayetakiwa tutakuwa tayari kumuachia,” alisema Manara.

Mkataba wa Kichuya uliobaki ni chini ya mwaka mmoja na kwa kiwango chake uongozi wa Simba unaona ni bora wamuuze sasa kama itapatikana timu kuliko kusubiri wakati mkataba wake ukimalizika anaweza kukataa kusaini mkataba mpya hivyo kuondoka bure kama ilivyokuwa kwa Ibrahim Ajib.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →