Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Simba wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza Singida United bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la Namfua mkoani Singida.
Ikicheza ikiwa tayari imetwaa ubingwa msimu huu, Simba ilijipatia bao pekee kwenye dakika ya 24 mfungaji akiwa Shomari Kapombe akitumia vyema makosa ya Salum Chukwu aliyerudisha mpira mfupi langoni kwake.
Mpaka mapumziko Simba ilitoka dimbani ikiwa inaongoza kwa bao hilo pekee.

Kipindi cha pili ni Singida United iliyotawala kwa muda mwingi ikisaka bao la kusawazisha lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Simba pamoja na mlinda lango Aishi Manula uliwawezesha mabingwa hao wa ligi kuondoka na ushindi muhimu uliowafanya waendeleze rekodi ya kutofungwa wakiwa sasa wamebaki na michezo miwili.
Licha ya kuwa ugenini ni mashabiki wa Simba waliofurika kwenye uwanja wa Namfua na kuwafunika kabisa wenyeji wao waliokuwa wapole kama wamemwagiwa maji hasa baada ya timu yao kufungwa.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo wachezaji wa Singida United waliwapa heshima mabingwa Simba kwa kuwapigia makofi wakati wanaingia dimbani.

Awali uongozi wa Singida United ulidai usingefanya zoezi hilo la kimichezo linalofanywa kote duniani kwa timu bingwa.

ADVERTISE HERE