Simba imetwaa ubingwa wa VPL ikiwa safarini mkoani Singida baada ya Yanga kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Prisons jana.
Simba iliondoka jijini Dar es salaam mapema asubuhi ya jana Alhamisi na ilipofika mkoani Dodoma iliweka kambi ya muda katika hoteli ya Golden Crown.
Mshambuliaji kinara wa mabao Emanuel Okwi pamoja na nahodha wa Simba John Bocco waliongoza shamrashamra za kutwaa ubingwa hotelini hapo.
Simba itakuwa mkoani Singida leo kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Singida United kesho kwenye dimba la Namfua.
Wachezaji wa Simba wameapa kulinda rekodi yao ya kutofungwa msimu huu licha ya kuwa tayari wameshatwaa ubingwa.

ADVERTISE HERE