Licha ya kuwa tayari imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, wachezaji na benchi la ufundi la Simba wameitahadharisha Singida United kuwa ijiandae kupokea "kichapo" katika mechi itakayowakutanisha kesho kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.
Singida United na Simba zinakutana katika mechi ya raundi ya 28 huku wenyeji wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema kuwa, kwao kila mechi ni sawa na fainali na hawatapunguza "spidi" mpaka watakapofika mwisho wa msimu.
Djuma amesema japo tayari wametwaa ubingwa, watafurahi kuona wanaweka rekodi ya kutofungwa na kuchukua tuzo mbalimbali zitakazotolewa.
"Msimu una mechi 30, tumecheza 27 na zimebakia tatu, nazo tunataka kushinda na tunajiandaa kama tulivyokuwa tunajiandaa katika mechi zilizopita, mazoezi na nia yetu ni kutopoteza mchezo hata mmoja," alisema kocha huyo raia wa Burundi.
Simba ilisafiri jana kwenda mkoani Singida tayari kwa mchezo huo, ilitwaa ubingwa wakti iko safarini baada ya Yanga kulazwa mabao 2-0 na Tanzania Prisons.

ADVERTISE HERE