Wekundu wa Msimbazi, Simba ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2017/18 wakitwaa ubingwa wakiwa njiani kuelekea mkoani Singida.
Kipigo cha mabao 2-0 ilichopata Yanga kutoka kwa Prisons leo, kimekuwa ngazi ya Simba kuufikia ubingwa huku ikiwa na michezo mitatu mkononi.

Yanga yenye alama 48 imebaki na michezo mitano ambayo hata wakishinda yote watafikisha alama 63 wakati tayari Simba ina alama 65.
Jumamosi, May 12 Simba itakuwa mkoani Singida kuchuana na Singida United katika mchezo ambao sasa utakuwa wa kwanza kusherehekea ubingwa msimu huu.

ADVERTISE HERE