Pluijm aahidi kuipa mtihani Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 May 2018
Pluijm aahidi kuipa mtihani Simba
Kocha Mkuu wa Singida United Hans van Pluijm amesema mchezo wao dhidi ya mabingwa watarajiwa wa ligi kuu ya Vodacom Simba watautumia kulipa kisasi cha kipigo katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza.

Singida United itakuwa nyumbani keshokutwa May 12 ikiikaribisha Simba kwenye mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Namfua.

Katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Simba iliifumua Singida United mabao 4-0.

Pluijm amesema mawazo yao yote wameyaelekeza kwenye mchezo huo ambao Simba inaweza kutwaa ubingwa kama haitapoteza iwapo Yanga itashinda dhidi ya Prisons leo.

Simba ina nafasi ya kutwaa ubingwa leo kama Prisons itaweza kuifunga au kutoka sare na Yanga.

Mchezo kati ya Singida United na Simba unatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote.

Simba inahitaji kupata matokeo yatakayoiwezesha kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa msimu huu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’