Simba isipotangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wikiendi hii, itatangaza pale Taifa kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar wiki moja baadaye.
Hesabu zinaonyesha hivyo kwani vinara hao wanahitaji pointi mbili tu kujitangazia ubingwa wao.
Sasa habari njema ni kuwa kocha wa timu hiyo yenye pointi 65 kileleni, Pierre Lechantre, tayari ameanza mipango ya kufanya usajili wa maana kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Lechantre amekifanyia tathimini kikosi chake kwa muda wa miezi minne aliyokaa akichukua mikoba ya Joseph Omog na kubaini anahitaji usajili wa nyota kadhaa tu ili kupata kikosi cha kushindana kwenye mashindano ya kimataifa.
Amesema atafanya usajili wa washambuliaji wawili wa maana mmoja akiwa wa kigeni mwenye uwezo wa kufunga zaidi ya Emmanuel Okwi na John Bocco.
"Nataka mshambuliaji mwingine mzawa mwenye uwezo wa kufunga kama Okwi na Bocco ili kuongeza makali kikosini. Unajua tangu nimefika hapa nimekuwa ninawategemea zaidi Okwi na Bocco,†alisema kocha huyo wa zamani ya Cameroon.
“Sawa wamekuwa na maelewano mazuri na wamefanya kazi vizuri, hakika wanastahili pongezi.
“Nataka kuongeza pia nguvu kwa kufanya usajili wa kiungo mkabaji ambaye kwa sasa yupo mmoja tu katika timu yangu, jambo ambalo si salama katika msimu ujao ambao tutakuwa na mashindano mengi ambayo tumedhamiria kufanya vizuri.
“Hayo ni mapendekezo ambayo yatakuwa kwa upande wangu, lakini nitakaa na benchi langu la ufundi kusikia nao wameona kitu gani na baada ya hapo tutakabidhi ripoti ambayo itakuwa imekamilika kila kitu.â€
Ligi itakapomalizika, kabla ya Lechantre kuondoka kwao Ufaransa kwa ajili ya likizo, pamoja na benchi la ufundi la Simba watafanya kikao na bilionea, Mohammed Dewji ‘MO’ ambacho kitakuwa kinahusu mambo mawili makubwa.
Jambo la kwanza litakuwa kuifanyia kazi haraka ripoti ambayo itahusu wachezaji ambao watahitajika kwa ajili ya msimu ujao, pili ni mpango wa kutafuta wachezaji vijana.
“Nilivyofika hapa Simba katika mambo ambayo tulikubaliana ni kuwa na timu nzuri ya vijana ili kuibua wachezaji wazuri na tulikubaliana na Dewji. Tutalianza hilo mara baada ya msimu huu kumalizika,†alisema.
Wakati huo huo, nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella, amesema Simba inatakiwa kutafuta straika mmoja atakayewaongezea nguvu, Bocco na Okwi, lakini pia atafutwe kiungo mmoja na beki wa kuhakikisha ulinzi unakuwa imara zaidi.
“Simba ijifunze kuwa na mtazamo wa mbali, iaache sifa za ligi za ndani, nashauri watulize akili kupata wachezaji watatu wenye viwango vya juu na makini zaidi ndipo tutapiga hatua michuano ya kimataifa,†alisema.
“Sababu ya kutolewa na Al Masry katika Kombe la Shirikisho Afrika, ilitokana na uwepo wa wachezaji wachache wenye moyo wa kujitolea na kushindwa kuwa makini kitu kilichopelekea kukosa maamuzi ya kupata matokeo.â€
Pia aliwataja Shomary Kapombe na Shiza Kichuya kwamba wameonyesha moyo wa kutaka timu ifanikiwe kwa namna ambavyo walikuwa na roho ya uzalendo, akisema kwamba ndio kitu kilichowafanya wawe nguzo katika kikosi cha kwanza cha makocha wote waliofundisha kwa msimu huu.
“Kuna kitu cha tofauti ambacho nimekiona kwa Kapombe na Kichuya, walivaa uhusika kama wachezaji halisi wazawa,†alisema.
“Kwangu mimi wanastahili pongezi na wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho la kipekee na viongozi.
“Ni wachezaji halisi wanaopaswa kuwamo katika timu.â€
Kwa hisani ya Mwanaspoti

ADVERTISE HERE