Mastaa walion'gara kwenye kikosi cha Simba msimu huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 May 2018
Mastaa walion'gara kwenye kikosi cha Simba msimu huu
Emanuel Okwi

Mabao yake 20 mpaka sasa yamemuweka kileleni kwenye mbio za kuwania ufungaji bora msimu huu, hakuna shaka atatwaa kiatu cha dhahabu.

Okwi ameifanya safu ya usambuliaji ya Simba ime moto wa kuotea mbali.

John Bocco

Wakati anasajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu wapo walioponda usajili wake. Wengi waliamini umri wake pamoja na majeraha ya mara kwa mara vingeigharimu Simba.

Lakini haikuwa hivyo, Bocco amekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya Simba msimu huu.

Uwezo wake wa kuzifumania nyavu pamoja na uzoefu wa muda mrefu wa soka la Tanzania kwa kiasi kikubwa vimechangia kuifanya Simba iweze kutwaa ubingwa msimu huu.

Bocco ndiye anayemfuatia Okwi kwa mabao kwenye ligi akiwa na mabao 14.

Shiza Kichuya

Msimu uliopita Kichuya alizoeleka akicheza kwenye wingi ya kulia na alipachika mabao mengi akitokea upande huo.

Hata hivyo baada ya kuondoka aliyekuwa kocha wa Simba Joseph Omog, Kocha msaidizi Masudi Djuma alibadili mfumo wa uchezaji wa Simba na alianza kumtumia kama kiungo mshambuliaji.

Licha ya kuwa amefunga mabao saba msimu huu, Kichuya ndiye kinara wa kutengeneza mabao kwenye ligi. Mguu wake umechangia jumla ya mabao 27 ya Simba(kafunga 7, usaidizi 20)

Masudi Djuma

Huyu aliletwa Simba kumsaidia Joseph Omog baada ya kuondoka kwa Jackson Mayanja.

Hata hivyo baada ya kuondolewa Omog, Djuma alikabidhiwa timu kwa muda wakati Simba ikisaka kocha wa kudumu.

Djuma ndiye aliyebadili mfumo wa uchezaji wa Simba na kuanza kutumia walinzi watatu nyuma. Licha ya sasa kuwa chini ya Pierre Lechantre, Djuma ndiye aliyeifanya Simba kuwa hivi ilivyo.

Aishi Manula

Huyu ndiye mlinda lango bora wa Tanzania kwa sasa. Amekuwa bora kwenye kikosi cha Simba. Hajaruhusu bao kwenye michezo 18 ya ligi.

Erasto Nyoni

Nyoni ameleta utulivu kwenye safu ya ulinzi ya Simba. Uwezo wake wa kucheza namba zaidi ya moja umewarahisishia walimu wa Simba kumtumia kulingana na mahitaji ya mchezo.

Jonas Mkude

Hakuwa akipata nafasi sana wakati Simba ikinolewa na Omog. Lakini tangu kuondoka kwa Omog, Mkude amedhihirisha yeye ndiye kiungo bora wa ukabaji nchini.

Simba imekuwa ikipata wakati mgumu Mkude anapokosekana dimbani. Yeye amekuwa bosi wa safu ya kiungo ya Simba.

Asante Kwasi

Kwasi alisajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo la usajili katikati ya mwezi Novemba 2017 akitokea Lipuli FC.

Muda mfupi aliokuwa kwenye kikosi cha Simba ameweza kudhihirisha ubora wake. Mabao yake matatu aliyofunga Simba yamemfanya kufikisha jumla ya mabao nane na kuwa beki mwenye mabao mengi zaidi msimu huu.

Shomari Kapombe

Tangu arejee kikosni mwanzoni mwa mwaka huu, Kapombe amedhihirisha kuwa mabosi wa Simba walifanya uamuzi sahihi kumsajili.

Aliposajiliwa mwanzoni mwa msimu alikumbwa na majeraha yaliyomuweka nje kwa karibu miezi sita hali iliyowakatisha tamaa baadhi ya mashabiki.

Lakini sasa kwa kiasi kikubwa mchango wake umeisaidia Simba kutwaa ubingwa msimu huu.

Yusuph Mlipili

Tangu aanze kutumika kama beki wa kati, amekuwa na kiwango kizuri na kumfanya kuwa beki wa kutumainiwa wa kikosi cha Simba.

Amekuwa na uelewano mzuri anapocheza na Erasto Nyoni kwenye safu ya ulinzi ya Simba.

Pierre Lechantre

Huyu ndiye kocha Mkuu wa kikosi cha Simba. Jambo moja kubwa alilofanya tangu atue Simba ni kutovuruga utaratibu uliokuta ambao uliasisiwa na Msaidizi wake Masudi Djuma.

Alichokifanya Lechantre ni kuboresha zaidi mfumo alioukuta ili kuimarisha zaidi kikosi cha Simba.

Lechantre alibadili majukumu ya baadhi ya wachezaji kama Shomari Kapombe ambaye sasa ni kiungo na hata wakati mwingine kumtumia Asante Kwasi kama kiungo pia.

Utaratibu wake huo umeweza kuimarisha mfumo wa kujilinda wa kikosi cha Simba.

Japo kumekuwa na malalamiko kwamba mfumo wake ni wa kujihami zaidi kuliko kushambulia, lakini ukweli unabaki palepale Simba imekuwa ngumu zaidi kufungika wakati huu lakini pia inaendelea kushinda michezo yake.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
10h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
10h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
13h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’