Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba wamebakisha alama moja tu ili waweze kutwaa ubingwa msimu huu.
Wakiwa na alama 65 na mtaji mkubwa wa mabao ya kufunga, alama moja itawafanya wafikishe alama 66.
Ni Yanga pekee yenye ubavu wa kufikisha alama 66 lakini itahitaji kufunga zaidi ya mabao 21 katika michezo yake sita iliyosalia ili kuweza kufikia idadi ya mabao ya Simba.
Hilo sio jambo jepesi na bila shaka kwa kiwango cha Yanga sasa, halitawezekana.
Simba inaweza kutwaa ubingwa Alhamisi hii May 10 kama Yanga itashindwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo dhidi ya Prisons utakaopigwa mkoani Mbeya.
Lakini kama Yanga haitairahisishia Simba, basi vinara hao wa ligi wamepania kumaliza kazi wenyewe Jumamosi watakapochuana na Singida United.
Simba inatarajiwa kusafiri katikati ya wiki hii kwenda mkoani Singida tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 28 dhidi ya SIngida United.
Kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema kikosi chake kimepania kutwaa ubingwa bila ya kupoteza mchezo hivyo watahakikisha hawaharibu rekodi hiyo mkoani Singida.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, Simba iliilaza Singida United kwa mabao 4-0

ADVERTISE HERE