Mshambuliaji kinara wa mabao katika kikosi cha Simba Emanuel Okwi anahitaji kufunga bao moja tu ili kuifikia rekodi ya mabao 21 iliyowekwa na Amissi Tambwe misimu miwili iliyopita kwa wachezaji wa nje.
Jana Okwi alifunga bao lake la 20 kwenye mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na hivyo kuukaribia kabisa ubingwa.
Takwimu zake msimu huu zinambeba Okwi na bila shaka atakuwa mfungaji bora.
Anayemfuatia kwa mabao kwenye ligi ni nahodha wa Simba John Bocco mwenye mabao 14 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Marcel Kaheza mwenye mabao 13.

ADVERTISE HERE