Kocha msaidizi wa Simba, Mrundi Masudi Djuma leo ameshuhudia mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya timu hiyo na Njombe Mji akiwa jukwaani, huku sababu ya kibali cha kazi ikitajwa.
Masudi aliyewasili juzi kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiondoa katika timu hiyo kwa madai ya matatizo ya kifamilia, alianza kazi ya kuinoa Simba kwenye mazoezi ya timu hiyo juzi jioni na jana asubuhi, huku mashabiki wengi wakiamini kuwa angekuwepo benchi katika mchezo wa leo kusaidiana na kocha mkuu Joseph Omog.
Hata hivyo kocha raia wa Burundi alionekana akiwa jukwaani akifuatilia mchezo huo kwa makini na kuishushia Simba ikifanya mauaji kwa kutoa kipigo cha mabao 4-0 kwa Njombe Mji wakati jina lake likiwa katika lineup ya timu hiyo.
Mashabiki wa klabu hiyo sasa itabidi kusubiri kuona mbwembwe za kocha huyo benchi katika mchezo ujao dhidi ya mahasimu wao Yanga utakaofanyika Oktoba 28 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Awali jana Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda alisema wanaendelea kufuatili kama kocha huyo msaidizi wa Simba ametimiza taratibu zote za kufanya kazi nchini.
"Sheria iko wazi kuwa mgeni yoyote anapoingia nchini awe mchezaji au kocha lazima afuate taratibu za kupata kibali cha kazi na ukaazi. hivyo Simba na Yanga zinaelewa hizo taratibu kwamba mgeni akija kufanya kazi nchini lazima kwanza aende Wizara ya Kazi kupata kibali cha kazi kisha akilete Uhamiaji ili kupata kibali cha ukaazi.
"Bado hatuna uhakika kama huyo kocha wa Simba ametimiza taratibu hizo tunaendelea kufuatilia," alisema Mtanda

ADVERTISE HERE