Sherehe za ubingwa na zianze sasa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 May 2018
Sherehe za ubingwa na zianze sasa
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC jana, Simba sasa inahitaji angalau alama moja kutoka michezo mitatu iliyobaki ili iweze kutwaa ubingwa.

Simba pia inaweza kutwaa ubingwa bila hata ya kushuka dimbani kama Yanga itashindwa kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Prisons May 10.

Simba ikiwa na alama 65 ni miujiza pekee itayoifanya isitwae ubingwa msimu huu.

Pongezi za kipekee wanastahili wachezaji na viongozi wa Simba kwa kufanikisha kutwaa ubingwa msimu huu.

Viongozi wa Simba wamefanikiwa kusajili kikosi imara pamoja na kuleta walimu wenye uwezo mkubwa wa kufundisha soka.

Kuletwa kwa Pierre Lechantre ambaye amewahi kutwaa ubingwa AFCON mwaka 2000 akiwa na timu ya Taifa ya Cameroon, kunadhihirisha dhamira ya dhati waliyokuwa nayo viongozi.

Baada ya kuukosa ubingwa kwa misimu mitano hatimaye sasa furaha imerejea Msimbazi na hakika imestahili.

Simba ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu na inayo nafasi ya kumaliza michezo yake mitatu iliyobaki bila ya kufungwa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
16h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
19h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’