FT : Simba 1-0 Ndanda FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 May 2018
FT : Simba 1-0 Ndanda FC
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba wamezidi kuusogelea ubingwa baada ya kuichapa Ndanda FC bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Bao pekee la Simba kwenye mchezo huo lilifungwa na Emanuel Okwi kwenye dakika ya 43 akipiga shuti nje kidogo ya 18.



Okwi ameongeza idadi yake yake ya mabao akiongoza mbio za kuwania ufungaji bora sasa akiwa na mabao 20.

Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe alama 65 na sasa huenda ikahitaji alama moja tu kuweza kutwaa ubingwa msimu huu.

Yanga yenye alama 48 na michezo sita inaweza kufikisha alama 66 kama itashinda yote lakini Simba imefunga mabao mengi zaidi, imefunga mabao 21 zaidi ya Yanga.

Haitakuwa jambo jepesi kwa Yanga kushinda michezo yote sita iliyobaki, achilia mbali kufunga mabao 21 kwenye michezo hiyo.

Mchezo unaofuata wa Simba ni dhidi ya Singida United May 12 kabla ya kuivaa Kagera Sugar na kisha kumaliza msimu dhidi ya Majimaji.

Katika michezo mingine iliyopigwa leo Azam FC imelazwa mabao 2-1 na Stand United, Majimaji imelazimishwa suluhu ya bila ya kufungana na Mtibwa Sugar kadhalika Kagera Sigar na Mbeya City nazo zimetoka suluhu
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’