Simba imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kwa tofauti ya mabao mengi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji.
Ikicheza katika dimba lake la nyumbani, Uwanja wa Uhuru Simba iliwafunza soka la kitabuni vijana wa Njombe Mji waliojuta kuwafahamu wekundu wa Msimbazi.
Emanuel Okwi ndiye aliyeanza kuifungia Simba bao la kuongoza hilo likiwa bao lake la nane msimu huu.

Baadae Mzamiru Yassin akapachika mabao mawili kabla Laudirt Mavugo hajafunga kalamu ya mabao kwa bao safi la kichwa akimalizia krosi ya Shiza Kichuya kutoka upande wa pili.
Licha ya kufunga, Okwi alitengeneza moja ya mabao ya Mzamiru.
Simba ingeweza kufunga mabao zaidi kama safu ya ushambuliaji ingeongeza umakini.

Baada ya mchezo huo benchi la ufundi la Simba limeelekeza nguvu zake kwenye mchezo ujao dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 28.
Kwingineko Mtibwa Sugar imefanikiwa kuilaza Prisons bao 1-0 hivyo kuendelea kuipa changamoto Simba kilelni ambapo timu zote zimefikisha alama 15.
Matokeo ya michezo mingine;

ADVERTISE HERE