Niyonzima arejea tayari kuivaa Ndanda FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 May 2018
Niyonzima arejea tayari kuivaa Ndanda FC
Simba inahitaji pointi tano tu kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu na kiungo wao Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas' aliyekosa mechi dhidi ya Yanga, amerudi kuungana na wenzake na kupigania ubingwa huo waliukosa kwa takribani miaka mitano.

Niyonzima amerudi akitokea kwao Rwanda alipokuwa kwenye msiba wa dada yake anayeitwa Sumaye jambo lililomsababishia akakosa mchezo dhidi ya Yanga mwishoni mwa mwezi uliopita.

Amerudi na kukuta timu yake inahaha kusaka pointi tano ambazo zitawatangaza kuwa mabingwa msimu huu na hiyo ni baada ya kucheza mechi 26 na kuvuna pointi 62 sasa wanahitaji hizo tano ili wafikishe 67 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yeyote.

Yanga ndiyo timu pekee wenye nafasi ya kuwapindua Simba kama watapoteza mechi zao baada ya kucheza mechi 24 na kufikisha pointi 48, wakishinda mechi zao zote sita zilizobaki watakuwa na 66 na ndiyo nafasi yao pekee.

Kwani Azam inayowafuata nyuma, wao wameshautema rasmi ubingwa huo kwa sababu mechi 26 walizocheza wamepata pointi 49, hata wakishinda zote nne zilizobaki watakuwa na 61 tu.

Meneja wa Simba, Richard Robert amesema: "Haruna amesharudi na kuungana na wenzake kwenye timu kwa ajili ya maandalizi ya michezo mingine ijayo. Ameshaanza mazoezi na wenzake na kila kitu kinakwenda sawa."

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
11h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
12h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
15h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’