Simba yasaka rekodi mechi zilizobaki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 May 2018
Simba yasaka rekodi mechi zilizobaki
Benchi la ufundi la Simba limesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wameendelea kufanya mazoezi magumu kwa ajili ya kuikabili Ndanda FC kwa sababu wanataka kucheza kwa kasi na nguvu ya hali ya juu kwenye mechi hiyo na nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizobakia msimu huu.

Simba inatarajia kuikaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayofanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema kuwa kila mechi kwao ni muhimu na hatua waliyofika ina changamoto zaidi ukilinganisha na kule walikotoka.

Djuma amesema kila timu inahitaji kumaliza vizuri msimu na kurekebisha makosa ilivyofanya kwenye mechi za awali na kujitengenezea "ulaji" kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Tunataka kuona kasi yetu ni ile ile, tunajiandaa kama kawaida tunavyojiandaa kucheza mechi nyingine," alisema kwa kifupi Djuma, kocha wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda.

Alisema wachezaji wote wa timu hiyo wanafahamu kwamba wanatakiwa kutodharau wapinzani wao na kupambana mpaka mechi ya mwisho ya ligi.

"Tunajua bado hatujamaliza safari yetu, tunahitaji kushinda taji la ligi na vile vile kuwa na matokeo bora zaidi, kila mmoja anataka kuweka rekodi iliyo bora kwa ajili ya kujenga heshima," alisema kocha huyo.

Baada ya mechi dhidi ya Ndanda FC, Simba itasafiri kwenda Singida kuwafuata wenyeji Singida United na kurejea kuwasubiri Kagera Sugar halafu itaenda Songea kumaliza msimu kwa kuwavaa Majimaji.

Vinara hayo wa ligi wanahitaji pointi tano tu ili watangazwe rasmi kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Simba inaweza kuweka rekodi ya kutopoteza mchezo msimu huu kama haitafungwa kwenye michezo minne iliyobaki
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’