Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) katika kikao chake kilichofanyika juzi Mei Mosi, 2018 chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga kilipitia matukio na malalamiko mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Kamati hiyo imemsimamisha mlinzi wa Yanga Kelvin Yondani aliyemtemea mate beki wa Simba Asante Kwasi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Simba dhidi ya Yanga.
Kamati hiyo imelipeleka suala la Yondani kwa Kamati ya Nidhamu ambayo itatoa maamuzi itakapokutana.
Kamati hiyo pia imemuonya Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara kwa kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.
Kamati imesema kitendo chake ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

ADVERTISE HERE