Ngorongoro Heroes yaanza maandalizi kuikabili Mali

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 May 2018
Ngorongoro Heroes yaanza maandalizi kuikabili Mali
Timu ya soka ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), itawakaribisha yosso wenzao kutoka Mali katika mechi ya kwanza ya kusaka tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika itakayopigwa Mei 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ngorongoro Heroes ilisonga mbele katika mashindano haya baada ya kuwaondoa yosso wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa penalti 6-5 kufuatia kutoka suluhu kwenye mechi zote mbili.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alisema maandalizi ya mechi hiyo yanaendelea vyema na kikosi cha Ngorongoro Heroes kinachonolewa na Kocha Mkuu, Ammy Ninje, kinaendelea na mazoezi yake ambayo wanafanya mara mbili.

Ndimbo alisema ili kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani, TFF imepanga kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa ni Sh. 3,000 kwa eneo la VIP na Sh. 1,000 kwa watakaokata viti vya mzunguko.

"Kikosi hicho hakina majeruhi na vijana wako katika morali kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika," alisema Ndimbo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’