Kichuya apanda thamani, timu kibao zamtaka

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 May 2018
Kichuya apanda thamani, timu kibao zamtaka
Mkataba wa Shiza Kichuya wa kuitumikia Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu na inaelezwa kiungo huyo amegoma kusaini mkataba mpya hadi mkataba wake wa sasa umalizike.

Simba italazimika kufanya kazi ya ziada kumshawishi Kichuya kuendelea kucheza Msimbazi msimu ujao kwani tayari kuna timu nyingi zinamuwania.

Habari za uhakika zimebainisha kuwa kuna timu kutoka nchini Algeria inamtaka Kichuya huku ikiweka mezani ofa ya mshahara wa zaidi ya Mil 20 kwa mwezi.

Kichuya anahusishwa pia kutakiwa na TP Mazembe na timu kutoka Misri na Afrika Kusini huku hapa nchini Azam FC ikielezwa kumyatia winga huyo aliye katika kiwango bora.

Mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Wachezaji wengine ambao mikataba yao ya kuitumikia Simba inamalizika mwishoni mwa msimu ni pamoja na Mohammed Ibrahim 'Mo', Mzamiru Yassini na Said Khamis Ndemla.

Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah amesema klabu yake itaanza kushughulikia masuala ya usajili baada ya kujihakikishia imetwaa ubingwa.

"Kwa sasa tumeelekeza nguvu zetu zote kwenye mbio za ubingwa. Tukishamaliza hili basi tutakuwa na nafasi ya kuzungumzia masuala ya usajili."

Ligi kuu ya Vodacom inatarajiwa kumalizika May 26 2018.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’