Baada ya mapumziko ya siku mbili kikosi cha leo kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 27 dhidi ya Ndanda FC.
Mchezo huo utapigwa Jumapili ijayo May 06 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa mkoani Mtwara, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mazingira ya mchezo huo sasa yako tofauti kwa kuwa Ndanda nayo inapigana kufa na kupona ili kuhakikisha inabaki Ligi Kuu huku Simba ikihitaji kushinda kuusogelea zaidi ubingwa
Kibarua kigumu kwa Ndanda ni kuizuia Simba yenye kiu ya ubingwa ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita iliwatandika mabingwa watetezi wa Yanga baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Ndanda ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 huku ikicheza jumla ya michezo 26.
Mechi ya Simba dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa inatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na umuhimu wa mchezo huo kwa kila timu.

ADVERTISE HERE