Simba inahitaji alama tano tu kujihakikishia kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu.
Kwa maana nyingine ni kwamba simba inahitaji kushinda michezo miwili tu itwae ubingwa mapema.
Jumapili itacheza mchezo wake wa kwanza kati ya minne iliyosalia dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Taifa.
Kama itashinda mchezo huo utakaopigwa May 06 basi itahitaji kupata ushindi dhidi ya Singida United ili kutangaza ubingwa ikiwa na michezo miwili mkononi.
Mchezo dhidi ya Singida United utapigwa May 13 mkoani singida.
Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema mchezo dhidi ya Singida United utakuwa mgumu kutokana na uimara wa timu hiyo hivyo tayari wameanza mikakati ya kuhakikisha wanapata ushindi.
"Tuliwafunga hapa Dar es Salaam mabao manne, lakini hiyo haimaanishi wana timu mbovu au tutapata ushindi kirahisi, tunajua mchezo utakuwa mgumu na ndio maana tunajiandaa dhidi yao na hata Ndanda FC ambao tutaanza kucheza nao hapa," amesema Djuma.

ADVERTISE HERE