Ushindi mwembamba waliopata Simba dhidi ya Yanga mwishoni mwa wiki umemfanya kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djouma kutoa sababu ya matokeo hayo.
Kabla ya mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kikosi cha Simba kilionekana kuwa moto huku mashabiki wao wakiamini historia ya mabao 5-0 ingejirudia lakini ikawa tofauti.
Simba ilinyamazisha mashabiki wa Yanga kwa bao 1-0 lililofungwa na beki Erasto Nyoni akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu dongo uliopigwa na Shiza Kichuya nje ya 18 baada ya Kelvin Yondani kumchezea faulo Shomari Kapombe dakika ya 37.
Kocha Msaidizi wa Simba, Djouma alisema isingekuwa rahisi kufunga mabao mengi kutokana na aina ya mchezo wenyewe.
"Unajua hii ni derby, uwezekano wa kufunga mabao mengi inategemea na mpira ulivyowakubali na nafasi mlizozipa, Simba tulikuwa na shida hasa na pointi tatu siyo mabao mengi.
"Ndiyo maana tulipanga tusifunguke sana hasa baada ya kupata bao ili tusije kuruhusu sare na mbinu yetu ilifanikiwa," alisema Djouma.
Alisema japo mashabiki walidhani baada ya Yanga kupata kadi nyekundu ingewapa nafasi zaidi ya wao kushambulia, lakini haikuwezekana kwa kuwa baada ya kadi ile Yanga walijituma zaidi.
"Ni kama walicheza 'dabo' baada ya kadi, kwani mara zote timu inapocheza pungufu inajituma mara mbili na ndicho kilichotokea Yanga, kama nilivyosema hatukutaka kujihatarisha na kupoteza pointi tatu ndiyo sababu hatutukutaka kufunguka sana."
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE