Ilikuwa lazima tuwafunge - Nyoni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 May 2018
Ilikuwa lazima tuwafunge - Nyoni
Beki wa kutumainiwa wa Simba Erasto Nyoni amesema alifahamu timu yake itaifunga Yanga kwenye mchezo uliopigwa juzi uwanja wa Taifa.

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 huku Nyoni akifunga bao hilo pekee lililoipa Simba pointi zote tatu muhimu.

Nyoni amesema amekuwa na furaha baada ya kufunga bao hilo na kusema tangu awali walikuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.

"Nilifahamu mapema tutashinda mchezo ule, lakini sikufikiria kama nitafunga, tulipanga kupambana kuhakikisha tunashinda, ushindi huu ni wa Wanasimba wote," alisema Nyoni aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Azam FC.

"Mchezo na Yanga umepita, sasa tunajipanga kwa mchezo ujao, tutapambana kuhakikisha tunapata ushindi kwenye michezo yote iliyobaki," aliongeza kusema Nyoni.

Bao alilolifunga Nyoni juzi linakuwa la tatu msimu huu kuifungia Simba

Kwa ushindi wa juzi, Simba sasa itatakiwa kushinda michezo miwili tu kuweza kutawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.

Endapo Simba itashinda mechi hizo mbili, itafanikiwa kutwaa ubingwa bila kupoteza na kabla ligi haijamalizika kama ilivyofanya Barcelona ya Hispania juzi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’