Wakati ikielezwa beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, huenda akakumbana na adhabu ya kufungiwa mechi mbili na faini juu ama zaidi kutokana na kitendo chake cha kumtemea mate ('makohozi') beki wa Simba, Asante Kwasi amemsamehe kwa roho safi.
Kwasi akizungumza baada ya mchezo wa juzi amesema yaliyotokea amemuachia mungu.
Katika mechi hiyo ya watani wa jadi Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Saloum Chama, amesema alishuhudia kitendo hicho, lakini kamati yake itatoa uamuzi kwa kuzingatia ripoti ya mwamuzi, kamisaa au ushahidi wa picha za video ambazo zitawasilishwa.
Chama alisema, pia kwa kuzingatia uzito wa tukio lililojitokeza, kamati yake inaweza kumsimamisha kwa muda na kulipeleka katika Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili wachukue hatua ambayo wanaamini itakuwa ni fundisho kwa wachezaji wengine wasirudie.
"Kanuni zinasema kosa kama lile ni kufungiwa kati ya mechi moja au mbili au kupigwa faini, au kupata adhabu zote kwa pamoja, na kwa kuangalia uzito wa jambo husika, tunaweza kumsimamisha na kumpeleka katika Kamati ya Nidhamu," alisema Chama ambaye pia ni mwamuzi mstaafu.

ADVERTISE HERE