Ushindi wa bao 1-0 iliyopata Simba dhidi ya Yanga leo una maana kubwa kwa vinara hao wa ligi ambao sasa wanaweza kuanza kuandaa sherehe za ubingwa msimu huu.
Ni hivi, alama 62 ilizonazo Simba zinaweza kufikiwa na Yanga pekee iliyo nafasi ya tatu tena kama itashinda viporo vyake viwili.
Yanga imebakisha michezo sita ambayo kama wakishinda yote wanaweza kufikisha alama 66 hivyo kimahesabu Simba inahitaji alama tano tu kutangaza ubingwa.
Ikishinda michezo miwili itakuwa imetwaa ubingwa, hata ikishinda mmoja na kutoka sare miwili itakuwa imemaliza kazi!
Simba inaweza kuingia kwenye historia ya timu zilizomaliza msimu bila ya kupoteza mchezo kama haitafungwa kwenye michezo yake minne iliyobaki.

ADVERTISE HERE