Wekundu wa Msimbazi, Simba leo wamekata mzizi wa fitina baada ya kuwalaza wapinzani wao wa jadi Yanga kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Simba iliyokuwa mwenyeji wa mchezo huo, iliuanza mchezo taratibu lakini ilishika kasi baada ya dakika 10 za mwanzo na kutawala kwa muda mwingi.
Bao pekee la Simba liliwekwa kimiani na beki Erasto Nyoni kwenye dakika ya 37 akiunganisha krosi ya Shiza Kichuya kutoka upande wa kushoto.
Simba ilikwenda mapumziko ikiongoza kwa bao 1-0.
Katika kipindi cha pili ni Simba iliyoendelea kutawala, hata hivyo kwa kiasi kikubwa walinzi wa Yanga Kelvin Yondani na Andrew Vicent waliweza kuinusuru timu yao isipate kipigo kikali.
Kwenye dakika ya 47 beki wa Yanga Hassani Kessy alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Asante Kwasi na kuzawadiwa kadi ya pili ya njano.
Matokeo hayo yameusogeza ubingwa mikononi mwa Simba kama itashinda michezo miwili tu kati ya minne iliyosalia.
Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 62, alama 13 zaidi ya Azam FC iliyo nafasi ya pili na alama 14 zaidi ya Yanga iliyo nafasi ya tatu.
Ni muujiza pekee utayoifanya Simba isitwae ubingwa msimu huu baada ya ushindi dhidi ya Yanga.

ADVERTISE HERE