Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre amesema amekuwa akiifuatilia Yanga kwa muda sasa na sasa atatumia udhaifu wao kwenye mchezo wa kesho uwanja wa Taifa.
Lechantre alikuwepo uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Singida United uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Amesema Yanga ina wachezaji watatu ambao ndio muhimili wa timu hiyo.
"Kelvin Yondan, Thaban Kamusoko na Obrey Chirwa kuwa ndio wamekuwa wakihusika mara nyingi kwenye ushindi wa Yanga na kwamba, kila mmoja ana uwezo wake," amesema.
“Chirwa ana matumizi mazuri ya nguvu, msumbufu na ana uwezo wa kufunga ndio maana alipata nafasi moja tu katika mechi tuliokutana nao mzunguko wa kwanza na kufunga bao la kusawazisha.
“Mbali na kuyaona hayo kupitia luninga, pia nilipata muda wa kuitazama Yanga mubashara dhidi ya Singida United, nilikuwa uwanjani na mengi ambayo siwezi kusema hadharani kwa sasa niliyaona.
"Nimewapatia vijana wangu na ndio itakuwa silaha yetu uwanjani ya kuwachapa Yanga mapema tu.
“Yote haya nimeyafanya ili kuhakikisha tunapata ushindi ili kujiweka vizuri na ubingwa msimu huu, tunachukua ubingwa na hilo halina ubishi kabisa.â€

ADVERTISE HERE