Manara awaita mashabiki uwanja wa Taifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Apr 2018
Manara awaita mashabiki uwanja wa Taifa
Mkuu wa kitengo cha Habari klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa keshokutwa kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

'Derby' hiyo ya watani wa jadi itapigwa keshokutwa Jumapili, April 29.

Akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa Makao Makuu ya Simba mtaa wa Msimbazi, Manara amesema mashabiki wa timu hiyo hawajawahi kuiangusha Simba unapokuja mchezo wa watani wa jadi.

Amewataka kuendeleza utaratibu huo kwa kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti Simba ili iweze kuibuka na ushindi.

"Tunatarajia washabiki wetu siku hiyo waje kwa wingi sana wajaze uwanja kwa sababu sisi ndio timu tunayoongoza kujaza uwanja"

"Tufike kwa wingi, tuisapoti timu yetu kwa kushangilia kwa nguvu bila ya kufanya vurugu."

Manara pia amewakosoa waandishi wa habari wanaotumia neno MAHASIMU wa jadi kuwa hilo sio neno sahihi la kulitumia wanapozungumzia mchezo wa simba na Yanga sababu linamaanisha uadui.

"Mwandishi au mtu atakayesema sisi ni mahasimu na Yanga, atakuwa amenikosea sana. Sisi hatuna uhasama na hiyo ni lugha ya hovyo hovyo, sisi ni wapinzani tu, sisi ni watani wa jadi na upinzani wetu ni wa kawaida tu uwanjani ila sio mahasimu."

Manara amewataka waamuzi wa mchezo huo kuhakikisha wanachezesha kwa kufuata sheria 17 za soka.

Ò€œHuko nyuma ni wazi waamuzi walikuwa na mbeleko, lakini kwa sasa kuna mabadiliko. Kuna makosa madogodogo ya kibinadamu," amesema.

"Waamuzi wa pambano letu ni wa kimataifa na hata mashabiki wakija uwanjani waelewe kwamba makosa ni ya kibinadamu japo ubinadamu usiegemee upande mmoja.

"Kuhusu waamuzi wa nje, kanuni ziko wazi ni lazima waamuzi wawe wa Tanzania Bara (sio hata Zanzibar), kwa nchi kubwa kama Misri wanaleta waamuzi wa nje lakini kwa sasa inabidi tufuate sheria zilizopo".
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’