Tumerejea mapema tupate muda wa kupumzika - Djuma

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Apr 2018
Tumerejea mapema tupate muda wa kupumzika - Djuma
Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema wamerejea mapema kutoka mkoani Morogoro walikokuwa wameweka kambi ili wapate muda wa kupumzika.

Simba imerejea jijini Dar es salaam jana mchana.

Djuma amesema pia wanahitaji kufanya mazoezi ya mwisho kesho jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwavaa Yanga.

Djuma amesema asilimia 95 ya programu ya mazoezi kuelekea mechi hiyo wameshaifanyia kazi na sasa kilichobakia ni kuwakumbusha kila mmoja kutimiza jukumu lake anapokuwa uwanjani.

Kocha huyo raia wa Burundi alisema kuwa mechi hiyo inaonekana ngumu kwa sababu inahusishwa timu kongwe, lakini kiufundi, wameshacheza mechi ngumu zaidi msimu huu.

"Sina mengi ya kusema, ninachoomba ni kuendelea kuomba Mungu ili tutimize malengo yetu, tumecheza mechi nyingi ngumu na zenye ushindani kuliko, tuko tayari kwa mechi hiyo," alisema mchezaji huyo wa zamani wa APR ya Rwanda.

Simba mbali na kuongoza ligi ikiwa na pointi 59, inashikilia rekodi ya kutofungwa hata mechi moja katika msimu huu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
15h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’