Simba inaendelea kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga mkoani Morogoro sasa ikitumia uwanja wa Chuo cha Biblia baada ya kutokea mkanganyiko juu ya matumizi ya uwanja wa Highlands.
Ni siku tatu pekee zilizosalia kabla ya mpambano huo ambao huenda ukaiwezesha Simba kuanza sherehe za ubingwa mapema kama itaibuka na ushindi.
Simba inaongoza ligi kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Yanga, ushindi utaifanya ijikite kileleni kwa tofauti ya alama 14.
Hata kama Yanga itashinda michezo yake yote miwili ya kiporo haitakuwa na ubavu wa kumpata Mnyama kileleni kama ushindi utapatikana Jumapili.
Kocha Pierre Lechantre pamoja na Msaidizi wake Masudi Djuma wamekuwa wakisisitiza kwa wachezaji umuhimu wa mchezo huo kuelekea ubingwa msimu huu.
Katika mchezo huo Simba itamkosa kiungo wake fundi Haruna Niyonzima ambaye amesafiri kwenda nchini Rwanda kuhudhuria msiba wa dada yake aliyefariki jana.

ADVERTISE HERE