Simba na Yanga uso kwa uso Morogoro

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Apr 2018
Simba na Yanga uso kwa uso Morogoro
Wakati Simba ikiwa tayari mkoani Morogoro ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga, watani zao hao nao wametua mkoani humo kujiandaa na mchezo unaotarajiwa kupigwa Jumapili ijayo, April 29 2018.

Simba iliwasili Morogoro ikitokea Iringa baada ya mechi yake dhidi ya Lipuli FC wakati Yanga wametua mkoani humo jana baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City jijini Mbeya.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa timu yao imeweka kambi Morogoro na wanaamini ni mahali sahihi kwa lengo la kuwajenga wachezaji wake kuelekea mchezo huo wa Jumapili.

"Timu iko Morogoro, hali ya hewa na mazingira ya kambi ni rafiki, tunaamini benchi la ufundi litapata kile ilichokihitaji kuelekea mchezo wetu dhidi ya watani zetu," alisema Manara.

Naye Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema kuwa kikosi cha Yanga kilitarajiwa kuwasili Morogoro jana jioni tayari kuanza mazoezi ya kuwavaa watani zao.

"Tunaenda kuweka kambi Morogoro," alisema kwa kifupi meneja huyo.

Timu hizo zitakutana huku kila upande ukiwa na kumbukumbu ya kutoka sare katika mechi ya mzunguko wa kwanza wakati Simba yenye pointi 59 ikiwa kileleni ikifuatiwa na Yanga wenye mechi mbili.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
57m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’