Matokeo ya Simba ya sare ya 1-1 dhidi ya Lipuli, yaliwashtua mashabiki wengi wa soka hasa Wekundu wa Msimbazi wenyewe ambao, kama wamenza kuingiwa woga katika mbio za kubeba ubingwa msimu huu, lakini nahodha wa kikosi hicho, John Bocco 'Adebayor' amewatoa hofu na kuwaambia wanapambana na watafanikiwa tu.
Bocco amesema, waachane na matokeo hayo waliyoyapata juzi kwenye Uwanja wa Samora na sasa wanajipanga kwa mechi nyingine zilizobaki ili kuhakikisha zote wanafanya vizuri.
"Ligi ngumu kama unavyoona ni mapambano haswa, lakini sisi tunaachana na hiyo sare kwa sababu imeshapita na sasa tunasonga mbele kuhakikisha mechi zilizobaki tunafanya vizuri," anasema Bocco, ambaye ni miongoni mwa mshambuliaji wanaosumbua kwelikweli kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa amefunga mabao 14 akizidiwa matano tu na pacha wake, Emmanuel Okwi.
Amesema, Simba bado inaendelea kupambana na kuhakikisha wanautwaa ubingwa huo msimu huu kwa sababu kila kitu kinawezekana.
Kutokana na matokeo hayo, Simba iliyofikisha pointi 59 imepunguza pengo dhidi ya Yanga wenye pointi 48 baada ya mchezo wao wa jana Jumapili dhidi ya Mbeya City uwanjani Sokoine mjini Mbeya na kutoka sare ya 1-1

ADVERTISE HERE