Mchezo wa mzunguuko wa 25 ligi kuu ya Vodacom kati ya Lipuli FC dhidi ya Simba umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Samora mkoani Iringa uliishuhudia Lipuli ikianza kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 31 kupitia kwa Adam Salama.
Simba ilirejea mchezoni kwenye dakika ya 66 pale Laudirt Mavugo alipoisawazishia baada ya mpira wa kona uliopigwa na Shomari Kapombe kuzagaa langoni mwa Lipuli kabla Mavugo hajakutana nao na kuujaza kimiani.
Sare hiyo bado inaiweka Simba kileleni kwa tofauti ya alama 12 baada ya kufikisha alama 59.
Simba sasa inarejea jijini Dar es salaam kuwasubiri watani wa jadi, Yanga April 29 2018

ADVERTISE HERE