Simba yasaka alama tatu Iringa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Apr 2018
Simba yasaka alama tatu Iringa leo
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom, Simba leo wako mkoani Iringa kuikabili Lipuli FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 25.

Simba inayoongoza ligi kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili, inahitaji ushindi ili kuweza kuukaribia zaidi ubingwa.

Sasa ikiwa na alama 58, matokeo ya ushindi yataifanya ifikishe alama 61 wakati Yanga inayoshuka dimbani mkoani Mbeya kesho kuikabili Mbeya City, ina alama 47.

Kikosi cha Simba kiko mkoani Iringa tangu juzi, jana kikifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Samora.

Katika mchezo huo Simba itamkosa kiungo wake mahiri Jonas Mkude anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Aidha wachezaji Aishi Manula na Emanuel Okwi watalazimikia kucheza kwa uangalifu sana kama watapangwa ili kuhakikisha hawapati kadi za njano.

Wachezaji hao tayari wana kadi mbili za njano kila mmoja, kadi ya tatu itawafanya wakose mchezo unaofuata dhidi ya Yanga April 29.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’