Simba hii kuifunga ufanye kazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
20 Apr 2018
Simba hii kuifunga ufanye kazi
Ukitazama vizuri kikosi cha Simba, utagundua kuwa kati ya wachezaji 11 wanaunda kikosi cha kwanza, saba ni mabeki na wanne waliobaki mmoja kipa na watatu tu ndiyo washambulia staili ambayo kwa timu pinzani kuwafunga lazima ufanye kazi ya ziada.

Kocha wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre amekuwa akiwachezesha wachezaji saba ambao, kiuhalisia ni mabeki na ikitokea wamepungua sita lazima wawepo katika timu.

Simba ambayo inamtumia mlinda mlango wao, Aishi Manula katika mechi zote za ligi, kutokana na mfumo wao wa 3-5-2 au 4-4-2 imekuwa ikiwachezesha mabeki wa kati asili watatu hadi wanne badala ya wawili kama zinavyofanya timu nyingine.

Piga ua katika kikosi cha Lechantre huwezi kuwakosa, Juuko Murshid, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Asante Kwasi mbali na hao Mfaransa huyo humjumuisha Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na James Kotei katika kikosi kimoja

Amefanya hivyo katika mechi tofauti ikiwemo ile ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwa kuwachezesha sita na watano waliobaki alikuwa mlinda mlango Aishi Manula, kiungo Jonas Mkude na John Bocco, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.

Akitumia mfumo wa 3-5-2 akichanganya na 4-4-2 Juuko, Mlipili na Nyoni walicheza nyuma na pembeni kulikuwa na Tshabalala pamoja na Kapombe, winga ya kushoto alicheza Kwasi, Mkude kati na kulia Kichuya wakati washambuliaji wa kati alicheza Bocco na Okwi na baadaye alimtoa Kwasi akamuingiza Kotei. Upo uwezekano mkubwa mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Lipuli wakacheza hivyo kwa sababu Lechantre amesisitiza hataki kupoteza nafasi hata moja.

Wakati mwingine Lechantre amekuwa akimchezesha mshambuliaji Nicholas Gyan kwenye beki lengo likiwa ni kutoa krosi nzuri za mwisho kutokea pembeni na washambuliaji wafunge na hata anapokuwa huyo, Kapombe huwa anampandisha kucheza kiungo.

Lechantre amesema: “Watu hawaoni kama tunacheza mpira wa kushambulia kutokana na mfumo wetu ambao ni 3-5-2, lakini mpira tunaocheza ni wa kushambulia pamoja na kuzuia.”

Kocha wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohamed ‘Bares’ amesema: “Kwa aina ya mfumo huu huo ambao Simba wanacheza iko wazi kocha anataka matokeo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →