Kiiza aipa Simba ubingwa msimu huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Apr 2018
Kiiza aipa Simba ubingwa msimu huu
Mshambuliaji wa zamani wa Simba Mganda Hamis Kiiza amesema Wekundu wa Msimbazi watatwaa ubingwa Ligi Kuu msimu huu.

Simba inaongoza na pointi 58, akifuatiwa na Yanga yenye pointi 47, Azam FC (46), Tanzania Prisons (37) na Singida United (36).

Kiiza anayecheza Al-Hilal ya Sudan alisema Simba inauwezo wa kutwaa ubingwa kwa asilimia 80, kwa sababu kuna kila dalili ya kikosi hicho kinachofundishwa na Mfaransa Pierre Lechantre kuutwaa na hizo 20 zilizobaki ndiyo zitakwenda kwa timu hizo nyingine ikiwemo Yanga.

"Simba ina nafasi ya kutwaa ubingwa kwani wapo kwenye morali wa hali ya juu, wapambana kuhakikisha wanafanikiwa kupata matokeo, lakini kitu kikubwa tu ni kwamba wasibweteka kutokana na kuongoza na wawaangalie wanaowafuata nyuma yao," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga.

Kiiza amekwenda mbali na kuuzungumzia mchezo wa Simba na Yanga ambao utachezwa Aprili 29 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa timu itakayojiandaa vizuri na kuonyesha nidhamu ya mchezo ndiyo atakayefanikiwa kushinda mechi hiyo.

"Ubingwa ni kitu kingine na kushinda mechi ya watani pia ni kitu kingine, kwani timu hizo zinapokutana hazijawahi kuisha kuonyesha ushindani kila mmoja akitaka mashabiki wake wafurahi," alisema Kiiza.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’