Wakati msimu wa ligi kuu ya Vodacom ukielekea ukingoni, tayari timu zimeanza kuangaza macho kwa wachezaji wanaoweza kuongezwa kwenye vikosi vyao.
Kulingana na Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba, Haji Manara, Simba nayo tayari imeanza kuwamulika baadhi ya wachezaji.
Manara ameliambia gazeti la Championi kuwa wachezaji Ditram Nchimbi wa Njombe Mji, Abdallah Mfuko (Mwadui FC), Idd Kipagwile (Azam) na Habib Kyombo (Mbao FC) wana sifa za kuichezea Simba
Aidha Manara amesema kutokana na kikosi chao kwa msimu huu kuwa bora, hawatarajii kukifanyia marekebisho makubwa katika kipindi kijacho cha usajili wa dirisha kubwa.
“Kwa sasa ni mapema mno kusema nani na nani amenivutia lakini wapo walionivutia mpaka sasa.
“Kuna straika mmoja namba tisa wa Njombe Mji mrefu hivi (Ditram Nchimbi) yule ni mchezaji wa aina ya John Bocco, pia yupo Idd Kipagwile wa Azam FC, ile ni mashine nyingine.
“Pia Habib Kyombo ana ‘footwork’ nzuri, lakini pia yupo beki mmoja hivi wa kati anacheza Mwadui (Abdallah Mfuko), hao ndiyo wamenivutia ingawa siwezi kusema moja kwa moja tutawasajili.
“Kwa sasa tunaangalia namna ambavyo tutachukua ubingwa wa ligi na nadhani tukishachukua hatutabadilisha kikosi chetu kwa kiasi kikubwa, lakini katika marekebisho hayo tutafuata ripoti ya mwalimu anataka nini ingawa sisi kama viongozi tunaona sehemu ambazo zina upungufu,†alisema Manara.

ADVERTISE HERE