Ubingwa kwanza mambo mengine baadae - Okwi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Apr 2018
Ubingwa kwanza mambo mengine baadae - Okwi
Washambuliaji wa Simba vinara wa mabap, Emmanuel Okwi na John Bocco, kwa nafasi tofauti juzi walisema kuwa, wanatumia nguvu zaidi kuisaidia timu yao ipate pointi tatu katika kila mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara na si kufikiria tuzo ya kiatu cha dhahabu.

Okwi amefikisha mabao 19 msimu huu wakati Bocco yeye ana magoli 14, baada ya kila mmoja kufunga katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons.

"Kila siku kwanza nawaza kuisaidia Simba ipate ushindi, kwangu malengo ni kutwaa ubingwa na si kiatu cha dhahabu," alisema Okwi.

Naye Bocco, nahodha wa kikosi hicho kinachoongozwa na Mfaransa, Pierre Lechantre, alisema kuwa kila anaposhuka uwanjani anahakikisha anajituma ili timu yake ishinde bila kujali nani atakayefunga goli.

"Kipaumbele changu huwa ni kuona Simba inapata ushindi, na ndiyo malengo ya timu nzima, na ili kutimiza hili, ninajaribu kupambana kufunga kila ninapopata nafasi, ingawa najua mechi zote tunazocheza ni ngumu," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam FC.

Kikosi cha Simba kiko safarini kuelekea mkoani Iringa tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaoufata dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa Jumamosi, April 21 kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’