Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre ameendelea kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake ili kukidhi aina ya nchezo anaoutaka.
Katika michezo kadhaa Lechantre amekuwa akiwatumia Shomari Kapombe na Asante Kwasi kama viungo na kuwaacha nje viungo asilia kama Mzamiru Yassini, Haruna Niyonzima na Said Ndemla.
Katika moja ya mahojiano yake, Lechantre amesema mfumo wake yeye ni wa kushambulia na kukaba kuanzia langoni kwa mpinzani wake timu inapokuwa haina mpira.
Hivyo anahitaji wachezaji wanaoweza kufanya kazi zote mbili.
Katika siku zake za mwanzo ndani ya klabu ya Simba Lechantre alisema mapema kuwa kulikuwa na udhaifu mkubwa katika kujilinda hasa timu inapokuwa haina mpira.
Na hii ni kutokana na kuwa na viungo ambao ni wazuri wakati timu ina mpira lakini hawaisaidii timu wakati haina mpira.
Pengine hii ndiyo sababu inayopelekea viungo Niyonzima, Mzamiru na Ndemla kujikuta wanaachwa nje kwenye kikosi cha Simba siku za hivi karibuni.
Hata hivyo maalumuzi ya Lechantre yanaonekana kuinufaisha zaidi Simba kwani tangu itoke sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mwadui FC, imeshinda michezo yote iliyofuatia.
Lechantre amesema atawatumia viungo hao kadiri atakavyoona inafaa.

ADVERTISE HERE