Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam wamejichimbia mkoani Morogoro kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Lipuli FC itakayopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora, Iringa
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema Simba itafanya mazoezi mkoani hapo na baadaye Ijumaa mchana wataelekea Iringa kwa ajili ya mchezo huo wa raundi ya 25.
Manara alisema wanaamini benchi la ufundi litatekeleza vyema programu yao na kuwaweka wachezaji tayari kwa mchezo huo wa marudiano.
"Timu imeshafika Morogoro na itakuwa hapo kwa muda wa kama siku mbili kwa lengo la kufanya mazoezi, unajua kambi ya Morogoro huwa na baraka sana kwa klabu yetu," alisema Manara.
Aliongeza kuwa wanahitaji kuona wachezaji wanaimarika zaidi kwa sababu wanahitaji kupata pointi tatu katika mchezo huo na kuendelea na mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
"Kila mchezo kwetu ni fainali, vijana watajifua ili kuwa imara zaidi, kwetu kila mechi ni sawa na fainali, hatutaki kupoteza pointi kwa sababu walioko nyuma yetu wanatukimbiza kwa kasi ile ile inayofanana," Manara aliongeza.
Katika mechi hiyo ya Jumamosi, Simba itamkosa kiungo wake, Jonas Mkude, ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Baada ya mchezo huo, Simba itarejea kuisubiri Yanga katika mchezo mwingine ambao utapigwa Aprili 29, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini.

ADVERTISE HERE