Vinara wa Ligi Kuu Simba wanahitaji pointi 15, ili kujitangazia ubingwa msimu huu, baada ya misimu mitano kuondoka patupu.
Simba wenye pointi 58 imecheza michezo 24 huku wapinzani wao, Yanga wakiwa nafasi ya pili na pointi 47, baada ya kucheza michezo 22.
Endapo Simba itashinda mechi zake tano itafikisha pointi 73, ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga endapo itashinda mechi zake zote nane zilizobaki.
Hata hivyo Simba wanaweza kuukosa ubingwa iwapo itapoteza michezo miwili na Yanga wakishinda michezo yao nane iliyosalia basi Simba wanaweza kuukosa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa sita mfululizo.
Yanga inashirikia rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara 27 huku Simba wakifuata kwa kutwaa mara 18.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amesema kiu yake ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Okwi aliyeifungia Simba juzi bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penalti dhidi ya Tanzania Prisons, uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, amefikisha jumla ya mbao 19.
Γ’β¬ΕKila ninapocheza nawaza kuisaidia timu sio kuwa mfungaji bora, nachotaka kwanza ni kuchukua ubingwa hayo mengine yakifuata sio mbaya,Γ’β¬Β alisema mshambuliaji huyo.
Okwi kinara wa ufungaji mabao Ligi Kuu Bara akifuatiwa kwa ukaribu na mshambuliaji mwenzake wa Simba, John Bocco mwenye mabao 14.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE