Manara amtambulisha Djuma

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Oct 2017
Manara amtambulisha Djuma
Klabu ya Simba leo Oktoba 19, 2017 imemtambulisha aliyekuwa kocha wa Rayon Sport ya Rwanda Masoud Djuma kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja ambaye jana ametangaza kuachana na klabu hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara mchana wa leo amemtangaza Masoud Djuma kuchukua nafasi ya kocha msaidizi katika klabu yao hiyo ya Simba na kuwaomba wanachama wa mashabiki wa Simba kumpa ushirikiano kocha huyo.

"Tunawaomba wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba mumpe ushirikiano kocha wetu Masoud Djuma yeye ndiye atakuwa msaidizi wa Kocha Omog kuanzia leo Oktoba 19, 2017 na pia tumeboresha benchi la ufundi kwa kumteua meneja mpya Richard Robert yeye anachukua nafasi ya Dkt Kapinga ambaye alikuwa meneja kwa muda tuliokuwa naye mfupi lakini amerudi kwa mwajiri wake nasi klabu tumeona turidhie" alisema Haji Manara.

Mbali na hilo Manara amekanusha taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kocha wao Mkuu Omog ameondoka klabuni hapo kwa sababu hajalipwa mshahara na kusema kuwa wao Simba hawajawahi kuwa na njaa na kusema kuwa kocha mkuu wao anaendelea na mazoezi na kikosi chao hivyo huo unaosambaa ni uzushi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
8h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’