Lechantre amjaribu kinda kutoka Ujerumani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
17 Apr 2018
Lechantre amjaribu kinda kutoka Ujerumani
Juzi mashabiki waliokwenda kutazama mazoezi ya Simba uwnaja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam walipigwa mshangao baada ya mgeni mmoja kuibuka kwenye mazoezi hayo akiwa sambamba na kocha, Pierre Lechantre.

Mgeni huyo alikuwa straika kinda wa Allience ya Ujerumani, Geofrey Kombole ambaye alifanya majaribio kikosini hapo wakati akisubiri dili kukamilika.

Lechnatre amesema kuwa Kombole ni straika matata na kama ataonyesha uwezo basi atakuwa mchezaji wa kwanza kumsajili.

Kambole alitumia saa 1:30 kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Simba chini ya uangalizi Lechantre na wasaidizi wake Masoud Djuma na Mohammed Habib.

Lechantre katika mazoezi ya Simba juzi Jumamosi aligawa timu mbili ya kwanza ikiwa na Said Mohammed ‘Nduda’, Vincent Costa, Ally Shomary, Salim Mbonde, Jamali Mwambeleko, Haruna Niyonzima, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo na Kombole.

Nyingine ilikuwa Emmanuel Mseja, James Kotei, Paul Bukaba, Kelvin Faru, Said Ndemla, Mohammed Ibrahim, Mohammed Hussein, Moses Kitandu, Juma Liuzio, Rashid Juma.

Baada ya kupangwa kwa timu hizo walicheza kama mechi dhumuni lilikuwa kuangalia uwezo katika kukaba na kushambulia kwani Lechantre alikuwa mkali kwa ambaye atafanya vibaya lakini kuangalia pia uwezo Kombole ambaye aliweza kufunga goli moja safi kumuacha Nduda akishangaa na alipokea pasi safi kutoka kwa Niyonzima.

Lechantre alisema alimuona Kambole katika mechi za vijana katika Uwanja wa JK Kidongo Chekundu akiwa anafanya mazoezi na alivutiwa na uwezo wake kwani, anapenda wachezaji vijana na alimwambia kabla ya kurudi Ujerumani afike kufanya mazoezi na Simba.

“Nilimuona akicheza vizuri katika mashindano ya vijana alinivutia na ndio maana nimemwambia kabla ya kuondoka kurudi Ujerumani afanye kwanza mazoezi na Simba, kama atafanya vizuri naweza kufanya kitu kwa ajili yake,” alisema.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Kambole alisema: “Lechantre aliniona pale JK na baada ya mashindano kumalizika aliniambia nifike hapa kufanya mazoezi.

"Nina uwezo wa kucheza katika timu yoyote na nitakaa hapa ataniangalia kama nitafanya vizuri au nitashindwa,” alisema Kombole.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →