Kuelekea mchezo wao wa wikiendi hii dhidi ya Njombe Mji, kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo ambao utapigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog, amesema, kikosi chake kinakabiliwa na kundi kubwa la wachezaji waliokuwa majeruhi huku mbele yake kuna mechi kubwa ikiwemo ile ya Yanga.
“Nikipindi kigumu tulichopo kwasasa asilimia kubwa ya wachezaji tegemeo wapo nje wakisumbuliwa na majeruhi na mbaya zaidi tunakwenda kukutana na timu kubwa zenye ndoto ya ubingwa kama ilivyo sisi hii ni hatari lakini hatuna cha kufanya zaidi ya kupambana,â€amesema Omog.
Kocha huyo amesema katika mchezo huo atawakosa wachezaji watatu muhimu ambao ni beki Salum Mbonde, John Bocco na Shiza Kichuya ambaye bado yupo kwenye hatihati ya kucheza au kutocheza kutokana na majeraha ya enka yanayomsumbua.
Kocha huyo aliyepo kwenye kipindi kigumu, kutokana na matokeo ya timu hiyo amesema hakuna njia nyingine zaidi ya kuwaamini wachezaji waliopo na kuwaimarisha ili waweze kucheza na kuisaidia timu yao iweze kupata matokeo katika mechi hizo.
Amesema watapambana kwasababu pamoja na majeruhi hayo lakini bado wanatimu nzuri ambayo inawachezaji wengi wenye vipaji ispokuwa kinachowasumbua ni uzoefu ukilinganisha na wale walioumia.
Simba ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 12, sawa na timu za Yanga, Mtibwa na Tanzania Prisons lakini yenyewe ikiwa na mtaji mkubwa wa mabao ya kufunga.

ADVERTISE HERE