Lechantre awawakia wachezaji Simba licha ya kushinda 3-1

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Apr 2018
Lechantre awawakia wachezaji Simba licha ya kushinda 3-1
Licha ya kupata ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyofanyika juzi dhidi ya Mbeya City, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Pierre Lechantre, hakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo huo.

Akizungumza baada ya mechi hiyo kumalizika, Lechantre, alisema kuwa amefurahi kupata pointi tatu na kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa, lakini wachezaji wake walishindwa kufuata maelekezo aliyowapa kuelekea mchezo huo.

Lechantre alisema kuwa hali hiyo ni hatari hasa pale inapotokea wakati timu yako ikiwa haijafunga bao lolote na mpinzani anapofanikiwa "kukubana" na kumiliki mpira na kusababisha kukosa ushindi.

"Sijafurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wangu, hawakufuata vyema maelekezo niliyotoa katika mechi hii (dhidi ya Mbeya City), waliwaruhusu kutawala na kuwazuia kuonyesha aina ya mfumo nilioupanga," alisema kocha huyo raia wa Ufaransa ambaye anasaidiwa na Masoud Djuma, kutoka Burundi.

Naye mshambuliaji kinara katika ligi hiyo, Emmanuel Okwi, alisema kuwa bado mbio zao za kuwania ubingwa zinaendelea kwa sababu pointi nane walizoachana na Yanga ni chache.

"Lengo langu kwanza ni kuisaidia timu, na siwezi kuzungumzia ubingwa kwa sababu Yanga tumewapita pointi nane lakini wao wanamechi mkononi, tunahitaji kupambana ili kuhakikisha tunafikia malengo," alisema Mganda huyo.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuendelea na mazoezi leo kwa ajili ya kujiandaa kuwakaribisha Tanzania Prisons katika mechi nyingine ya ligi hiyo itakayofanyika Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini huku ikiwa na kumbukumbu ya kuwafunga "Maafande" hao katika mechi ya mzunguko wa kwanza.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
19h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’