Simba imedondosha alama nyingine mbili mkoani Lindi baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Tatizo la mipira ya krosi limeendelea kuitafuna Simba kwani Namungo Fc leo wamefunga mabao mawili mepesi kupitia mpira wa kona uliofungwa na Massawe na krosi ya Lusajo iliyofungwa na Chirwa mbele ya walinzi wa Simba
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi lakini ilijikuta iko nyuma mapema tu kabla ya kusawazisha kwenye dakika ya 42 kupitia kwa Shomari Kapombe
Bao la pili la kusawazisha kwa Simba lilifungwa na Kibu Denis kwa shuti la nje kidogo ya 18
Kwa hakika sio matokeo mazuri kwa Simba, ni mchezo wa tatu mfululizo Simba inashindwa kupata ushindi kwenye ligi kuu
Huu umekuwa msimu mbaya zaidi kwa Simba kwani matokeo haya yanaweza kuwa yamezika kabisa matumaini ya Simba katika mbio za ubingwa
Tofauti ya alama dhidi ya Yanga ni 12 huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 21, imebaki michezo tisa tu