Salamba mchezaji bora wa VPL March

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Apr 2018
Salamba mchezaji bora wa VPL March
Mshambuliaji wa Lipuli ya Iringa, Adam Salamba amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Salamba ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salum Kimenya wa Prisons na kipa wa Azam, Mwadini Ally katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo hizo.

Mshambuliaji huyo kwa Machi alionesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake kupata mafanikio akifunga mabao matatu kwa dakika 270 alizocheza, ambapo Lipuli ilicheza michezo mitatu ikishinda miwili na kutoka sare mmoja na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya nane hadi ya saba kwa mwezi huo.

Kwa upande wa Kimenya alicheza dakika 269 na kufunga mabao mawili, akiiwezesha Prisons kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kutoka sare mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya tano hadi ya nne.

Mwadini yeye alicheza dakika zote 270 ambazo timu yake ilicheza kwa mwezi Machi, ikishinda michezo yote mitatu iliyocheza, ikibaki katika nafasi yake ya tatu.

Kutokana na ushindi huo, Salamba atazawadiwa tuzo, kisimbusi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil. Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).

Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco (Januari) na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari).
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’