Kiungo mshambuliaji wa Simba, Hassan Dilunga, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki nne baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini
Dilunga alipata majeraha ya goti wakati Simba ikijiandaa na mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas
Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco amesema upasuaji wa nyota huyo ulikuwa wa mafanikioΒ
Amesema anaamini Dilunga atarejea akiwa fiti baada ya kufanyiwa upasuaji huo
"Dilunga amefanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini na atakuwa nje kwa muda usiozidi wiki nne kabla ya kurudi tena uwanjani kuipambania timu," alisema Pablo