FT : Simba 3-1 Mbeya City

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Apr 2018
FT : Simba 3-1 Mbeya City
Wekundu wa Msimbazi, Simba wamepiga hatua moja zaidi kuukaribia ubingwa wa VPL msimu huu baada ya kuilaza Mbeya City mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 23 uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Simba ilifunga mabao yake yote matatu kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa vinara wake wa mabao kikosini, Emanuel Okwi (16'), Asante Kwasi (32') na John Bocco ('35).



Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Mbeya City lilifungwa na F. Khamis kwenye dakika ya 34 kwa mpira wa kichwa.

Okwi ndiye aliyeanza kuifungia Simba kwenye dakika ya 16 akimalizia mpira uliokuwa umepanguliwa na mlinda lango wa Mbeya City baada ya shuti la John Bocco.

Kwasi aliifungia Simba moja ya mabao mazuri msimu huu baada ya kuvunja mtego wa kuotea na kuwahi krosi iliyopigwa na Shiza Kichuya aliyetengewa mpira na Shomari Kapombe.



Nahodha wa Simba John Bocco alimalizia pasi murua ya Shomari Kapombe baada ya Simba kufanya shambulizi la kushitukiza.

Ushindi huo unaifanya Simba ijichimbie kileleni kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Yanga liyo nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 55.

Simba inashuka tena uwanja wa Taifa siku ya Jumatatu, April 16 kuikabili Tanzania Prisons.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’