Moto utawawakia Mbeya City uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Apr 2018
Moto utawawakia Mbeya City uwanja wa Taifa leo
Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wanatarajia kuwakaribisha Mbeya City FC kutoka Mbeya katika mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.

Simba itashuka katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Mbeya City yenyewe ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC.

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema kila mechi iliyo mbele yao ni sawa na fainali, hivyo wamejipanga kupambana kuhakikisha wanapata pointi tatu.

Djuma alisema mechi zote za ligi kuanzia mwanzo na zilizobakia ni ngumu na kila hatua inavyoendelea ndiyo ushindani unaongezeka zaidi.

"Tunafanya maandalizi kwa ajili ya kupata ushindi, kila mechi kwetu ni sawa na fainali, hakuna timu wala mechi nyepesi, na hatua ya sasa ni ngumu sana, ila kwa mapenzi ya Mungu, naamini tutafanya vizuri," alisema kocha huyo wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda.

Naye Kocha Mkuu wa Mbeya City, Nsanzurwino Ramadhani, alisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio kuwa vijana wake wako tayari kwa mchezo huo huku akiweka wazi kwamba anaiheshimu Simba.

"Simba ninaijua na nimeshaiona inavyocheza, tunajua sehemu ya kuwakaba ili kuwazuia wasipate matokeo, kama wanafuata nilichowaelekeza, natarajia hatutapoteza tena pointi," alisema kocha huyo.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 na ushindi kama huo pia ilipowavaa Tanzania Prisons uwanjani hapo.

Simba yenye pointi 52, ndiyo inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ambayo msimu ujao itashirikisha timu 20 na Mbeya City yenyewe iko katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 26.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
31m ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
19h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’